WATU WAWILI WANAO SADIKIWA KUWA NI WEZI WAUAWA JIJINI ARUSHA, NGARENARO

watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wezi wameuawa kwa kugongwa na gari katika mtaa wa nagarenaro jijini hapa juzi kuamkia jana,

Shuhuda akiongea na muandishi wetu katika eneo latukio alifunguka haya, ilikuwa ni saa tatu usiku watu tukiwa tumelala jirani yetu alikuwa akitoka katika mizunguuko yake akiwa na mwanae wa kiume katika gari yao wakati wanaingia nyumbani katika geti walivamiwa na watu zaidi ya 10 wakiwa na silaha wakati baba alikuwa ameshashuka katika gari ndipo walimvamia na kumchoma kisu mtoto aliyekuwa katika gari alifanikiwa kumgonga mmoja na kupelekea kifo chake na mwingine alimgonga nje ya nyumba yao na kupelekea kifo chake pia, jirani yetu yupo hospital ya maunti meru kwaajili ya matibabu. alisema shuhuda huyo

hii si mara ya kwanza matukio kama haya kujiri mkoani hapa tunaliomba jeshi la polisi kuweka umakini zaidi katika suala la usalama wa wananchi wake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post