WAZIRI AWAFUNDISHA WABUNGE JINSI YA KUMALIZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Wakati matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume yakazidi kushika kasi Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni, sakata hilo limetinga bungeni ambapo mmoja wa wabunge alitaka kujua hatua ambazo serikali inazichukua kukabiliana na tatizo hilo ambali si linawakumba wazee tu, bali hata vijana wadogo.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Hamis Kigwangalla alisema ni kweli kwamba tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa huku akitaja baadhi ya mambo ambayo wanaume wanatakiwa kuzingatia ili kuepuka au kuondokana kabisa na tatizo hilo.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Konde, Khatib Haji likihoji alihoji “Kumekuwa na ongezeko kubwa kwa tatizo la wanaume kupungukiwa nguvu za kiume Je, Serikali inajua tatizo hilo? na kama inajua inachukua hatua gani kukabiliana na tatizo hilo?”
Aidha, Mbunge huyo aliitaka wizara yenye dhamana kuzungumzia suala la utumiaji wa dawa kiholela kutoka na uwepo wa ongezeko la matangazo ya waganga na watu mbalimbali wanaodaiwa kuwa wanatoa dawa zinazoweza kuongeza nguvu za kiume.
Akijibu swali hilo, Dr. Kigwangalla alisema, anaunga mkono hoja hiyo kuwa, ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume umekuwa mkubwa lakini akawataka wanaume kufanya mazoezi, kula vizuri, kupata muda wa kutosha wa kupumzika ili kuweza kukabiliana na matatizo hayo ambayo ni hatari kwa afya ya uzazi.
“Napenda kutoa hamasa kwa wanaume wote nchini, kushiriki kwa kiasi kikubwa kwenye mambo yanayolinda afya zetu, kufanya mazoezi, kupumzika, kula vizuri lakini pia kufurahi, kucheka na kushirikiana na wenzako ili kuondoa msongo wa mawazo kwasababu msongo wa mawazo, sonono  wasiwasi ni katika vitu vinavyosababisha Erectile disfunction na hata kukosa watoto kwa wengine kushindwa kushika mimba…Naamini tukizingatia tutaweza kukabiliana na tatizo hilo.”
Kigwangalla aliwataka wanaume kuacha kuhangaika na dawa zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume na badala yake wahakikishe wana afya njema kwani suala la nguvu za kiume ni suala la mwili wako kuwa katika afya bora. Aidha, wanaotumia dawa ambazo hazijahakikiwa na Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA) wameonywa kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia madhara makubwa.
“Ukiwa na msongo na uchovu kwa hakika huwezi kuwa na ile hamasa ya kushiriki tendo la ndoa ipasavyo na hii ni sababu mojawapo na ndio maana nashangaa watu ambao wanahangaika sana kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume. Hiyo ni changamoto ya kimwili lazima uwe na afya njema, uwe huna magonjwa lakini pia hutumii madawa kwa muda mrefu lakini pia uwe umetulia, uwe na amani katika moyo wako na hiyo huwezi kupata raha kama huna furaha.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post