WAZIRI MKUU KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUANDAA MIPANGO, BAJETI NA RIPOTI

SHARE:

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO DODOMA:  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua  mfumo  wa kiel...

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
DODOMA: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua  mfumo  wa kielektoniki wa kuandaa Mipango , Bajeti na Ripoti kwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa(PlanRep) na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji  wa Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS).
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA Ofisi ya Rais – TAMISEMI Baltazar Kibola amesema kuwa mifumo hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Septemba 5, 2017 katika ukumbi wa LAPF Mkoani Dodoma.
Akifafanua Bw. Kibola  alisema kuwa lengo la mifumo hiyo ni kusaidia kuja na mfumo mmoja wa kitaifa utakaowezesha kuwa na utaratibu wa kuandaa mpango na bajeti ambapo utasaidia Hamlashauri zote nchini kuwa na muundo mmoja wa uandaaji wa mipango na Bajeti za Serikali.
Aidha alisema kuwa lengo la Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni kushirikiana na Serikali katika kuimarisha mfumo ili kusaidia uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa  katika ngazi ya kila kituo husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dkt. Gemin Mtei alisema kuwa lengo la mradi huo ni kufanya maboresho ya mifumo katika Sekta za Umma ili kuongeza ufanisi.
“Mradi huu unalenga kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Utawala Bora, Rasilimali watu, Rasilimali Fedha na pia katika maeneo ya TEHAMA ambapo utasaidia ni namna gani mifumo inawezeshwa kufanya kazi kwa urahisi” amesema Dkt. Mtei.
Aidha Dkt. Mtei amebainisha baadhi ya maeneo yaliyolengwa kufanyiwa maboresho ikiwemo utoaji wa huduma, kutambua watoa huduma na pia kuwekeza kwa watoa huduma ili kuwezesha wananchi kuweza kunufaika na huduma hizo.
Vile vile Dkt. Meti alisema kuwa Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa na Mfumo wa Uhasibu wa Utoaji  wa Taarifa za Fedha kwenye Vituo vya Kutolea Taarifa(FFARS) Mradi wa  (PS3) ikiwa ni mradi wa miaka mitano (2015 – 2020) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (USAID) kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Naye Mtaalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago amesema kuwa mfumo umeundwa kwa kuzingatia Ubora, Usimamizi wa fedha, ufanisi katika utendaji kazi wa umma, kupunguza gharama za usimamizi na utendaji wa kazi.
“Mfumo uliokuwa ukitumika awali ulitumia gharama nyingi, muda mwingi na pia ulihusisha watu wengi kukaa kusafiri kukaa pamoja sehemu moja, ila mfumo huu ulioboreshwa umerahisisha utendaji kazi na kupunguza gharama iliyokuwa ikitumika awali” amesema Rwamiago
Akibainisha faida za mifumo hiyo kwa Serikali Rwamiago amesema kuwa itawezesha ufuatiliaji kuanzia ngazi za vituo vya Afya, Zahanati na shule hivyo utawezesha  upatikanaji wa taarifa kutoka katika kila kituo kwa wakati.
Vilevile amesema kuwa mifumo hiyo  ina manufaa katika ngazi zote za utendaji hivyo itasidia uunganishaji wa Taarifa kuhusu fedha za Serikali kutoka katika ngazi ya vituo hadi Halmashauri mpaka ngazi ya Taifa.
“Mifumo hiyo imeandaliwa katika ubora kwa kuzingatia changamoto zilizokuwepo  awali kwa lengo la kuleta ufanisi katika utekelezaji wa kazi za Serikali” alifafanua  Rwamiago.
Mradi wa uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni mradi uliounganisha Mikoa yote ya Tanzania na Halmashauri zake ambapo wataalamu wa masuala ya Mipango, Bajeti,Waganga wakuu wa Wilaya, Makatibu Afya, Mweka Hazina kutoka katika kila Halmashauri wamepatiwa mafunzo kuhusu Mifumo hiyo.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAZIRI MKUU KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUANDAA MIPANGO, BAJETI NA RIPOTI
WAZIRI MKUU KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUANDAA MIPANGO, BAJETI NA RIPOTI
https://2.bp.blogspot.com/-d037UU4k4qE/WaztmQPJCOI/AAAAAAAAeSA/9DHk_ZBSy7Y8Dfru6Mnm-b9aEHPYJncYACLcBGAs/s1600/x1-5-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.WCQgHg2iZh.webp
https://2.bp.blogspot.com/-d037UU4k4qE/WaztmQPJCOI/AAAAAAAAeSA/9DHk_ZBSy7Y8Dfru6Mnm-b9aEHPYJncYACLcBGAs/s72-c/x1-5-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.WCQgHg2iZh.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/waziri-mkuu-kuzindua-mfumo-wa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/waziri-mkuu-kuzindua-mfumo-wa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy