WAZIRI WA AFYA AZINDUA UGAWAJI WA BIMA ZA AFYA KWA WAZEE WILAYANI UBUNGO

SHARE:

Na Mathias Canal, Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 a...

Na Mathias Canal, Dar es salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 amezindua Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya TP Sinza E Waziri Ummy alipongeza uongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa kutambua umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya kuwatambua Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu bila vikwao.
Alisema kuwa Wazee ni asilimia 5.6 ya wananchi wote wa Tanzania idadi ambayo kwa kiasi kikubwa inaleta msukumo wa nchi kuweka mifumo madhubuti ya kuhudumia Wazee ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa Huduma katika matibabu.
Alisema kuwa Jambo hilo ni kuzingatia ukweli kwamba Wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na umri mkubwa na mtazamo wa Jamii ambao umekuwa ukichangia ukiukwaji wa haki na maslahi ya Wazee katika ngazi mbalimbali.
Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeingia kwenye rekodi kwa kuwatambua Wazee wasio na uwezo kwani watapatiwa vitambulisho vitakavyo wawezesha kupata Huduma za matibabu Bure.
Mhe Ummy alisema kuwa Halmashauri zingine kote nchini zinapaswa kuanzisha haraka zoezi la kuwathamini Wazee kwa kuwapatia Huduma Bora za afya kabla ya kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee kote nchini kwa kuanzisha dirisha maalumu na wataalamu wa kuwahudumia Wazee.
Alitoa Rai kwa watoa Huduma wa Afya kuviheshimu vitambulisho wakati wote Wazee wanapoenda navyo kupatiwa matibabu huku akiwasihi Wazee kutumia vitambulisho hivyo kwa kuzingatia maelekezo sio kwa kuwapa watu wengine wasiohusika navyo.
Aidha Waziri Ummy ameahidi bima ya afya kwa watoto 100 wenye umri chini ya miaka 18 wanaoishi kwenye mazingira magumu wilaya ya Ubungo na uandikishwaji utaanza leo pia ameahidi kujenga wodi ya wazazi, watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya wilaya ya ubungo mara baada ya kusikia hotuba ya kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Ubungo.
Muheshimiwa waziri ameiomba jamii kujiunga na bima za afya za gharama nafuu ili kupunguza mzigo kwa halmashauri na kulinda afya za wananchi
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alisema kuwa lengo la uzinduzi huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma kuwa Wilaya ya Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020, sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 na sera ya Afya ya Mwaka 2007.
Mhe Makori alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha Wazee wote nchini wanapata Huduma Bora za afya bila vikwao hivyo Wilaya ya Ubungo imeanza na utoaji vitambulisho kea Wazee 7296 waliojiandikisha na zoezi hilo litakuwa endelevu.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa vitambulisho vya Tiba kwa Wazee alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imetekeleza agizo la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo vya Afya vya Umma kutenga dirisha na watumishi maalumu wa Afya kwa ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa Wazee.
Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Vituo 19 vya kutolea Huduma za afya ikiwa ni pamoja na Hospitali moja, Vituo vya afya vitatu, Zahanati 15, na Kliniki Moja ya Mama na Mtoto hivyo Vituo hivyo vyote vitaanza kutoa Huduma za matibabu kwa Wazee wasio na uwezo bila malipo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akizungumza wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu (Wa Tatu Kushoto) akionyesha vitambulisho vya Wazee akiwa na viongozi wengine wa Chama na serikali Wilaya ya Ubungo wakati wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na baadhi ya Wazee walioshiriki uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Ubungo Bi Maria Maliwa akisoma taarifa ya huduma za afya, Ustawi wa jamii na Msamaha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika uzinduzi wa vitambulisho vya msamaha kwa wazee wa Manispaa ya Ubungo.
 
Zoezi la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Mzee Ferooz Kafuru kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa
vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
 
Kalli amepongeza uongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo kwa kutekeleza ilani ya CCM ya ushindi yenye mkataba na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akiteta Jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo mara baada ya kuzindua Huduma ya Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Walaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisalimiana na Wazee waliofika kushuhudia zoezi la uzinduzi wa vitambulisho kwa Wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo lilifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu akimpatia Bi Theresia Mbimbo kitambulisho Cha matibabu wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Baadhi ya Wazee wa Halmshauri ya Manispaa ya Ubungo wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 
Madiwani wa Manispaa wakishuhudia zoezi la Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee. Zoezi hili limezinduliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu leo Septemba 4, 2017 

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAZIRI WA AFYA AZINDUA UGAWAJI WA BIMA ZA AFYA KWA WAZEE WILAYANI UBUNGO
WAZIRI WA AFYA AZINDUA UGAWAJI WA BIMA ZA AFYA KWA WAZEE WILAYANI UBUNGO
https://3.bp.blogspot.com/-dy1kkm4f5zw/Wa3TEpsmnLI/AAAAAAAAeUc/vhwqAwgzi9Ml2dRRDzKflolxvsLpF4n0gCLcBGAs/s1600/4-1.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-dy1kkm4f5zw/Wa3TEpsmnLI/AAAAAAAAeUc/vhwqAwgzi9Ml2dRRDzKflolxvsLpF4n0gCLcBGAs/s72-c/4-1.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/waziri-wa-afya-azindua-ugawaji-wa-bima.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/waziri-wa-afya-azindua-ugawaji-wa-bima.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy