Zari anajifunga Nilan, Diamond na Mobetto wanamtafuta Dylan

SHARE:

Diamond Platnumz wiki hii amemkubali mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobetto atwaye Abdul aka Dylan kuwa ni mwanae baada ya kumkataa mtoto huyo...

Diamond Platnumz wiki hii amemkubali mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobetto atwaye Abdul aka Dylan kuwa ni mwanae baada ya kumkataa mtoto huyo kwa lengo la kumficha mama watoto wake, Zari The Bosslady ambaye tayari amezaa naye watoto wawili, Princes Tiffah pamoja na Nilan.

Hamissa Mobetto akiwa na baba Diamond kwenye arobaini ya Dylan iliyofanyika siku chache zilizopita

Rais huyo wa WCB amedai alikubaliana na mwanamitindo huyo kulifanya jambo hilo kuwa siri ili kulinda heshima yake na familia kwa ujumla kitu ambacho hakikufanikiwa.

Leo Tuamua kurudi nyuma na kuangalia ni siku gani na wapi Diamond na Hamisa Mobetto walikutana na kufanya mchakato wa kupatikana kwa Dylan ikiwa mtoto huyo alizaliwa 8/ 8/ 2017 katika hospitali moja hapa jijini Dar es salaam.

Wataalamu wa afya wanasema mwanamke hujifungua mtoto baada ya miezi tisa toka siku ambayo mimba imeingia. Pia kuna baadhi ya wanawake hujifungua kabla ya siku hizo kutokana na matatizo ya kiafya ambapo mtoto anayezaliwa kipindi hicho uitwa njiti na huwa katika uangalizi maalumu.

Lakini mtoto wa Mobetto, Dylan amezaliwa kawaida kulingana na taarifa ambazo aliziweka wazi mwanamitindo huyo na kama ni hivyo basi wawili hao walivunja amri ya sita mwezi Novemba mwishoni mwaka 2016 au Disemba mwanzoni. Je swali lilipo ni wakati gani na wapi wawili hao walikutana, hebu tungalie matukio ambayo yalitokea mwezi Novemba na Disemba ambayo bila shaka yalikuwakutanisha wawili hao wakati Zari akikaribia kujifungua mtoto, Nilan, Disemba 6 2016.

Salome yawakutanisha.

Video ya wimbo ‘Salome’ ndio project ya kwanza kuwakutanisha wawili hao baada ya mwanamitindo huyo kucheza vitendo katika video ya wimbo huo.Licha project hiyo kuwaweka karibu zaidi wawili hao lakini mapaparazi waliufuatilia ukaribu wao na kugundua kuna kitu kinaendelea kati yao huku mashabiki wakibaki na kumbukumbu ya neno ‘project’ ambalo pia liliwakutanisha kimapenzi Diamond na Zari.

“Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm.

Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”


Naye mwanamitindo huyo alivunja ukimya baada ya kuona stori za mahusiano yao zinachukua sura mpya hasa hasa baada kuona picha zake zinasambaa mtandaoni akiwa chumba kinachofanana au alichowahi kukitumia zari na Diamond wakiwa Afrika Kusini.

“Hiyo sio kweli,” alisema Hamisa kwenye mahojiano na gazeti la The Citizen baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo.

“Pia sijawahi kuwa karibu na Diamond na siku ya kwanza tumekutana ilikuwa ni siku anazindua video ya Number 1 pale Serena,” aliongeza. “Tena wakati hiyo habari imeanza kusambaa nilikuwa nje ya nchi.” alisema Mobetto.


AFRIMA: Diamond na Mobetto watua Lagos Nigeria.


Novemba 6 mwaka 2016 zilifanyika tuzo za All Africa Music Awards, AFRIMA, Lagos Nigeria. Usiku wa tuzo hizo uliwakutanisha mastaa mbalimbali wa muziki wa mataifa akiwemo Diamond ambaye ali-perform usiku huo.


Katika usiku huo wa tuzo Diamond Platnumz aliibuka na ushindi wa nguvu wa tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa.

Tetesi zinadai muimbaji huyo alisafiri nchini humo na mwanamitindo, Hamisa Mobetto hivyo basi baada ya ushindi huo bila shaka muimbaji huyo alipokea mabusu moto moto kutoka kwa mwanamitindo huyo mwenye umbo na muonekano wa kuvutia.

“Wakati tunarudi Lagos tulikuwa na Hamisa Mobetto, Diamond alikuwa VIP na sisi tulikaa business class,” alisema mmoja kati ya watu wa crew yake akiweka sharti la kutokutajwa jina lake.


Hata hivyo mwanamitindo huyo hakuwa anapost chochote kuhusiana na tukio hilo huku wadau wa mambo wakidai huo ulikuwa ni mpango maalumu wa kulifanya jambo hilo kuwa siri.

Diamond atua Full Moon Party, Mayotte na Zimbabwe

Muimbaji huyo baada ya kurejea nchini Tanzania siku sita baadaye, Novemba 12 aliibukia kwenye show ya Full Moon Party iliyofanyika Kendwa Rocks, Zanzibar. Show hiyo ilikuwa ya aina yake kutokana na kuwakusanya watu kutoka mataifa tofauti tofauti. Hata hivyo haikujulikana kama pia show hiyo alisafiri na mwanamitindo huyo.


Novemba 24 Diamond alitua Mayotte nchini Ufaransa, ambapo alipokelewa kwa shangwe na watanzania ambao walijitokeza kwa wingi katika uwanja wa ndege wa mji huo. Muimbaji huyo alifanya show mbili ambapo moja ilikuwa ya kawaida na nyingine ilikuwa ya VIP.


Baada ya show hizo muimbaji huyo alielekea nchini Zimbabwe ambapo alifanya shows zaidi ya tatu na Disemba 5 2016 alisafiri na mama yake kwenda nchini Afrika Kusini sehemu ambayo Zari alikuwa anajifungua mtoto wake wa pili.

Tetesi za mimba ya Mobetto zaanza kuzagaa kwa kasi.

Ingawa kulikuwa na usiri mkubwa lakini mambo yalianza kubadilika kwa Mobetto, Juni 21 2017 tetesi za mwanamitindo huyo kuwa ana mimba ya Diamond zilizagaa kwa kasi.

Hata hivyo Diamond akihojiwa na kipindi cha Leo Tena Cha Clouds FM alikanusha kumpachika mimba mrembo huyo.

“Toka nimeshoot video na Hamisa Mobeto wimbo wa Salome, watu wamekua wakituhusisha pamoja, ujauzito wa Hamisa sio wangu. Jamani mwenye mimba si ajitokeze, si unajua hata mtu wake atakuwa anajisikia vibaya,” alisema rais huyo wa WCB.

Zari anajifunga Nilan, Diamond na Mobetto wanamtafuta Dylan

Zari the Boss Lady alijifungua Dylan Disemba 6 mwaka 2016, naye Hamisa Mobetto amejifungua 8/8/2017 kwa maana hiyo kama mwanamitindo huyo alijifungua baada ya kutimiza miezi 9, basi Diamond na Mobetto walikutana na kuvunja amri ya sita mwezi Octoba ama Novemba wakati Zari ana siku chache za kwenda kujifungua.

06th Dec 2016 03: 35am SA time...... 04: 35am EAST Time.... 02: 35am WEST Time.... 01: 35 am NORTH Time, A NEW STAR WAS BORN in NETCARE HOSPITAL / PRETORIA / SOUTH AFRICA.... unfortunately his parents Dad & Mom haven't agreed on the name.... that's why it even took time, to his advent to be on his parent's Social media Pages..... Let's wait and See, what @zarithebosslady & @Diamondplatnumz will ended up call him... (Tareh 6/ 12/ 2016 saa kumi na dakika 35 Staa Mpya wa akiume alizaliwa katika hospitali ya NETCARE iliyopo mjini Pretoria / South Africa... kutokana na wazazi wake kutofikiana Muafaka wa mtoto aitwe jina gani, ilipelekea mtoto huyo kuchelewa kupostiwa kwenye Mitandao ya kijamii ya Wazazi wake.... tusubiri tuone @zarithebosslady na @DiamondPlatnumz wataishia kumpa jina gani Mtoto wao...✍ )

A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Novemba 6 mwaka 2016 zilifanyika tuzo za All Africa Music Awards, AFRIMA, Lagos Nigeria ambapo muimbaji huyo alidaiwa kusafiri na Mobetto na kutoka na mahesabu haya huwenda Diamond na Mobetto walivunja amri ya sita Nigeria na kufanikisha kupatikana kwa mtoto Dylan. Je ni kweli wawili hao walikutana Lagos hebu na wewe jaribu kuchanganua na utoe maoni yako kwani kipindi hicho chote Zari alikuwa akijitazamia kujifungua nchini Afrika Kusini hivyo isingekuwa vizuri kwake kuzunguka pamoja na Diamond katika show zake mbalimbali.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: Zari anajifunga Nilan, Diamond na Mobetto wanamtafuta Dylan
Zari anajifunga Nilan, Diamond na Mobetto wanamtafuta Dylan
http://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/09/Mobetto-na-Baba-Diamond.png
https://i.ytimg.com/vi/_bPjsDcPHks/default.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/09/zari-anajifunga-nilan-diamond-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/09/zari-anajifunga-nilan-diamond-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy