BODI YA TPSC YAAGIZWA KUSIMAMIA UTOAJI WA ELIMU BORA KWA WATUMISHI WA UMMA

SHARE:

Na: Thobias Robert Bodi ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye ...

Na: Thobias Robert
Bodi ya ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) imetakiwa kuhakikisha inaimarisha utoaji wa elimu bora na yenye viwango kwa watumishi wa umma ili kuendana na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotaka watumishi wenye weledi na wenye maadili katika sekta za umma na binafsi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki alipokuwa akizindua Bodi ya washauri wa chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Kairuki ameeleza kuwa ni wakati sasa kwa chuo hicho kuwa mfano bora wa kutoa watumishi ambao watarejesha nidhamu, utumishi bora na uadilifu wa hali ya juu katika sekta za umma na binafsi ili kumaliza tatizo la watumishi wasio waadilifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu kama rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Henry Mambo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa bodi ya ushauri ya chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja na menejimenti ya chuo hicho wakati wa uzinduzi wa bodi ya chuo hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
“Chuo cha utumishi wa umma hapa nchini kilianzishwa kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, hivyo Bodi ya ushauri wa chuo cha utumishi wa umma wa Tanzania inalo jukumu la kuhakikisha kuwa lengo hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa,” alisema Waziri Kairuki.
Aliongeza kuwa bodi hiyo pia inalo jukumu la kutoa ushauri katika mipango yote ya maendeleo, kushauri na kupitisha mpango kazi na bajeti ya chuo pamoja na kufanya tathimini ya mwaka ya utendaji wa chuo na masuala mengine ya muhimu yanayopaswa kutolewa ushauri.
“Nina matarajio makubwa kwamba, mtatekeleza majukumu hayo na mengine ambayo sikuyataja lakini yameelezwa katika sheria husika ili kuhakikisha kwamba, chuo cha utumishi wa umma kinakidhi matarajio ya serikali pamoja na wadau na kuleta tija na ufanisi katika utumishi wa umma hapa nchini,” alifafanua Waziri Kairuki.
Katika hafla hiyo iliyojumuisha wajumbe waliomaliza muda wao pamoja na wale waloteuliwa Waziri kairuki alisema kuwa, chuo hakina budi kupunguza kozi zisizo na soko kwa ajili ya kutoa elimu kwa ufanisi na tija kwa wanafunzi kama ilivyo kusudi la kuanzishwa kwa chuo hicho ambalo ni kutoa elimu kwa watumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Charles Msonde wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Dkt. Charles Msonde (kulia) akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro.
Aidha Waziri Kairuki amewapa changamoto wajumbe wa bodi hiyo walioteuliwa katika bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia, uendelevu wa chuo (Sustainabilty), kujitangaza kwa chuo ili kuongeza idadi ya wanafunzi, kozi gani zinazoweza kuwavutia wanafunzi, kufanya tathmini ya wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo kama wanakidhi vigezo katika ofisi za waajiri wa ofisi za umma na zile za binafsi.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), Dkt. Henry Mambo alisema kuwa kwa sasa chuo hicho kimefanikiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi, kutoa machapisho mbalimbali ya ndani na nje, kuanzisha kozi za shahada na kuongeza idadi ya wahitimu.
Dkt. Mambo alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi takribani 58221, katika Nyanja za uongozi, menejimenti na utawala bora, chuo kinadahili na kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi wa umma na watumishi tarajali wapatao 132890 na kati ya hao watumishi wa umma wanatarajia kuwa 29240 ambayo ni sawa na asilimia 22.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angellah Kairuki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mara baada ya kuizindua mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha na: Eliphace Marwa)
Naye Mwenyekiti mteule wa Bodi hiyo Dkt. Charles Msonde alisema kuwa atashirikiana na wajumbe, watendaji na Wizara ya utumshi kuendeleza mafunzo bora kwa watumishi wa umma ili kuendana mabadiliko ya sayansi na teknoljia pamoja na uhitaji wa soko hapa nchini na nje ya nchi.
Bodi hiyo inaundwa na wajumbe sita ambao ni Dkt. Charlse Msonde (Mwenyekiti), na Prof. Bernadetha Killian,Bibi. Anna Maembe, John Ullanga, Solanus Nyimbi, Bi. Roxana Kijazi
Chuo cha utumishi wa Umma kilianzishwa mwaka 2000 kwa lengo la kutoa elimu na mafunzo kwa watumishi wa umma hapa nchini na nje ya nchi,chuo hiki kipo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  kina matawi sita katika mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam (Magogoni), Mtwara, Singida, Tabora na Tanga

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BODI YA TPSC YAAGIZWA KUSIMAMIA UTOAJI WA ELIMU BORA KWA WATUMISHI WA UMMA
BODI YA TPSC YAAGIZWA KUSIMAMIA UTOAJI WA ELIMU BORA KWA WATUMISHI WA UMMA
https://2.bp.blogspot.com/-qMrxQ4DegXY/WdYgVndWqJI/AAAAAAAAfgw/IhbSqIUxtpU3VugVBasfIPo-pgNMiwSDwCLcBGAs/s1600/xPix-01-2-768x512-750x375.jpg.pagespeed.ic.BcLylYu86p.webp
https://2.bp.blogspot.com/-qMrxQ4DegXY/WdYgVndWqJI/AAAAAAAAfgw/IhbSqIUxtpU3VugVBasfIPo-pgNMiwSDwCLcBGAs/s72-c/xPix-01-2-768x512-750x375.jpg.pagespeed.ic.BcLylYu86p.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/bodi-ya-tpsc-yaagizwa-kusimamia-utoaji.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/bodi-ya-tpsc-yaagizwa-kusimamia-utoaji.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy