KAMPUNI YA ULINZI YA SGA YAZINDUA NEMBO MPYA YA HUDUMA KWA WATEJA

SHARE:

Kampuni ya Ulinzi ya SGA imezindua nembo mpya ya huduma kwa wateja ikiwa ni sehemu ya maadhinisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Akizind...

Kampuni ya Ulinzi ya SGA imezindua nembo mpya ya huduma kwa wateja ikiwa ni sehemu ya maadhinisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Akizindua nembo hiyo mpya, Mkurugenzi Mtendagi wa SGA Tanzania, Eric Sambu alisema kampuni hiyo inaweka mikakati madhubuti ili kuendana na matakwa na mahitaji ya wateja wao hasa katika mazingira ya sasa ya biashara ambayo yanabadilika kila kukicha.
Alisema kuna mabadiliko mengi mno katika soko na hivi kulazimu makampunni mengi kufanya mabadiliko ili kuendanana na hali halisi na makampuni mengi bado hayajaweza kusimama imara.
Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania Eric Sambu (kushoto) na Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Muliro Jumanne Muliro wakati Kamanda huyo alipotembelea ofisi za SGA Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Ili kuendana na hali halisi ya sasa hivi ni lazima tuendane na mazingira yalivyo ili tuweze kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu,” alisema Sambu.
Alisema SGA inaadimisha miaka 33 nchini Tanzania huku ikiwa imepata mafanikio mazuri hasa katika miaka mitano iliyopita na kusisitiza kuwa wameweza kupata mafanikio haya kutokana na kuboresha utendaji kazi, kuwezesha wafanyakazi kupitia mafunzo mbalimbali katika vitengo vyote. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, chata hii mpya inamlenga mteja zaidi katika utendaji wa SGA.
“Mabadiliko ya hivi karibuni katika ufanyaji biashara Tanzania yametupa fundisho kubwa na nafasi ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wetu wote katika ngazi zote ili waweze kuwahudumia wateja vizuri zaidi na kukidhi matakwa mapya ya soko sasa hivi na hili kwetu sasa hivi limekuwa jambo la kawaida,”
Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania Eric Sambu na OCD wa Kawe, Jiliyo Simba wakikagua gwaride rasmi iliyoandaliwa na maaskari wa SGA waliohitimu mafunzo.
“Tunaendelea kuboresha mifumo yetu na kuwekeza zaidi katika teknolojia na rasilimali watu ili kuhakikisha tunafanya vizuri. Tumeweza kuhakikisha tunapata hati safi katika usimamizi wa ubora tangu mwaka 2001 (ISO certification on Quality Management System) na hivi karibuni tumepata hati safi ya afya na usalama (Occupational Health and Safety ISO 18001 Standard).”
Meneja wa Uhusiano wa Wateja wa SGA, Aikande Makere, alisema wanaamini chata hii mpya itahakikisha kuwa wateja na wadau wote wanapokea huduma wanayostahili kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia uaminifu, uwajibikaji, usawa na wepesi wa kubadilika kulingana na mazingira.
“Tunawashukuru wateja wetu wote ambao wamekuwa pamoja nasi hata katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa katika biashara,” alisema Aikande.
Walinzi wa SGA wakiwa katika gwaride maalumu baada ya kuhitimu mafunzo maalum.
SGA ndio kampuni kongwe ya binafsi ya ulinzi nchini Tanzania huku ikiwa imeajiri zaidi ya watanzania 5100 katika maeneo ambayo wanafanya biashara Tanzania. Wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo ulinzi kwa kutumia maaskari, ulinzi kwa kutumia umeme, huduma za dharura (emergency response), ufuatiliaji (tracking), usafirishaji wa mizigo na vifurushi (courier) na usafirishaji wa fedha.
“Tuna magari 222 na vituo 12 nchi nzima ambavyo vina mitambo ya kisasa na wafanyakazi waliobobea katika masuala ya ulinzi na tumehakikisha kuwa tuna miundombinu madhubuti ya kuwahudumia wateja wetu nchi nzima.” alisema Sambu.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: KAMPUNI YA ULINZI YA SGA YAZINDUA NEMBO MPYA YA HUDUMA KWA WATEJA
KAMPUNI YA ULINZI YA SGA YAZINDUA NEMBO MPYA YA HUDUMA KWA WATEJA
https://1.bp.blogspot.com/-XJAHvVKBvWM/WdkeM_rD73I/AAAAAAAAfkk/BtCTK_qv0Yw_OvEpofnmKmTg4kVDFc3BQCLcBGAs/s1600/SGA-1-750x375.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-XJAHvVKBvWM/WdkeM_rD73I/AAAAAAAAfkk/BtCTK_qv0Yw_OvEpofnmKmTg4kVDFc3BQCLcBGAs/s72-c/SGA-1-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/kampuni-ya-ulinzi-ya-sga-yazindua-nembo.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/kampuni-ya-ulinzi-ya-sga-yazindua-nembo.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy