MANISPAA YA TABORA YAAGIZWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA VIWANJA VYA CCM

SHARE:

Serikali imeuagiza  Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanamaliza tatizo la uvamizi wa Viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapind...

Serikali imeuagiza  Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanamaliza tatizo la uvamizi wa Viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na vile vinavyomilikiwa na taasisi nyingine na watu binafsi ili waweze kuviendeleza.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula wakati alipotembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara ya siku moja katika Chuo cha Ardhi Tabora.
Alisema kuwa ni vema Halmashauri zote zikahakikisha zinaondoa migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha watu wenye maeneo yao ambayo yamevamiwa au kugawia watu wengine ambao sio wamiliki kihalali wanawaondoa na kuwarejeshea watu au Taasisi ambazo ndio zinazomiliki maeneo husika.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa Mamlaka zinapochelewa kutatua migogoro ya ardhi zinasababisha tatizo kuzidi kuwa kubwa na kusababisha usumbufu kwa wamiliki halali.
Aidha Naibu Waziri huyo alizishauri taasisi na watu binafsi wanaomiliki maeneo yao kihalali kuhakikisha wanaweka alama ikiwa ni pamoja na kupanda mimea hata kama maeneo yao bado hajapimwa ili kupunguza migogoro.
Awali akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora kwa kiongozi huyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Janeth Kayanda aliomba Serikali kuwasaidia kuwarudishia viwanja vyao sita ambavyo vilivyomilikishwa kwa watu wengine.
Alisema kuwa kitendo hicho kimesababisha Chama kishindwe kupanga mipango mbalimbali ya kuendeleza maeneo husika kwa sababu ya kuwepo na wavamizi hao na hivyo kumuomba kusaidia katika kutafutia ufumbusi wa viwanja vyao ili waweze kutekeleza mipango waliokusudia katika viwanja hivyo.
Katika hatua nyingine Katibu huyo wa Mkoa alimwomba Naibu Waziri kuangalia jinsi ya kuwasaidia baadhi ya wakazi wa Tabora ambao ni miongoni mwa wale 402 ambao nyumba zao zinatarajia kubomolewa kupitisha ujenzi wa reli ya kisasa.
Alisema kuwa baadhi yao walipewa kimakosa  viwanja hivyo na Mamlaka zinazohusika na ugawaji wa viwanja na kufuata taratibu zote na kulipia lakini hivi sasa wanatakiwa waondoke lakini miongoni hawana tena uwezo wa kujenga hata kama wakipewa viwanja.
Naye Mkuu wa Mkoa Tabora Aggrey Mwanri alimwakikishia Naibu Waziri huyo kuwa atahakikisha kuwa wavamizi wote wa viwanja wa chama na vile vya  taasisi nyingine na watu binafsi wanaondolewa na kupewa wamiliki wake kihalali.
Kufuatia hali hiyo alimwagiza Mkurugenzi Mteandaji wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha ndani ya wiki mbili watu wote waliovamia viwanja vya Chama wanaondoka nay eye anapata taarifa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yuko mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Ardhi ya siku moja ambapo baada ya hapo atakwenda Singida na Morogoro.
Na Tiganya Vincent, Tabora

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MANISPAA YA TABORA YAAGIZWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA VIWANJA VYA CCM
MANISPAA YA TABORA YAAGIZWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA VIWANJA VYA CCM
https://4.bp.blogspot.com/-uW7YHy8Kx0s/WdzriGcstZI/AAAAAAAAftQ/2MjnQseuf7UEz55NVyBeGHA-jAX1q7aIQCLcBGAs/s1600/4.-FURSA-NI-JAMBO-MOJA-UTAYARI-WA-WANANCHI-WETU-NI-JAMBO-JINGINE-NIWAOMBE-WANANCHI-KWA-UJUMLA-WAO-WAWE-TAYARI-KUSHIKIANA-NA-WAWEKEZAJI.-NAIBU-WAZIRI-WA-ARDHI-NA-MBUNGE-WA-ILEMELA-DKT.-ANGELINA-MABULA..jpg
https://4.bp.blogspot.com/-uW7YHy8Kx0s/WdzriGcstZI/AAAAAAAAftQ/2MjnQseuf7UEz55NVyBeGHA-jAX1q7aIQCLcBGAs/s72-c/4.-FURSA-NI-JAMBO-MOJA-UTAYARI-WA-WANANCHI-WETU-NI-JAMBO-JINGINE-NIWAOMBE-WANANCHI-KWA-UJUMLA-WAO-WAWE-TAYARI-KUSHIKIANA-NA-WAWEKEZAJI.-NAIBU-WAZIRI-WA-ARDHI-NA-MBUNGE-WA-ILEMELA-DKT.-ANGELINA-MABULA..jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/manispaa-ya-tabora-yaagizwa-kuwaondoa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/manispaa-ya-tabora-yaagizwa-kuwaondoa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy