MBUNGE VITI MAALUMU IRINGA KUKARABATI SHULE ZA MSINGI ZA MANISPAA YA IRINGA

SHARE:

Mbunge wa viti maalamu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za m...

Mbunge wa viti maalamu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amefanya ziara kwenye baadhi ya shule za msingi za manispaa ya Iringa kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kusomea.
Akizungumza mara baada ya kumaliza zira hiyo ya wiki moja Kabati alisema kuwa amefanya ziara katika shule ya msingi Kihesa,Igereke,Mtwira na shule ya Kibwabwa na kubaini changamoto nyingi ambazo anaanza kuzitafutia ufumbuzi hivi karibuni.
“Nimejionea mwenyewe changamoto zilizopo na naona kama changamoto kwa asilimia kubwa zinafanana hivyo ni kazi yangu kuanza kutafuta njia ya kuanza kuzitatua changamoto hizo,” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa atakikisha anazikarabati shule hizo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kama nilivyofanya hapo awali katika shule za msingi za Azimio na Kigonzile ambazo kwa sasa zinaubora kama shule za watu binafsi.
“Kwa kweli wadau wamekuwa wakinisaidia kufanikisha swala la kukarabati shule za msingi zilizopo hapa manispaa ya Iringa ili kuhakikisha mazingira ya shule zote yanakuwa bora kama shule za watu binafsi,” alisema kabati
Aidha Kabati aliwataka viongozi wa serikali na viongozi wa kisiasa kuzitembelea shule hizo mara kwa mara ili kutatua matatizo haya mapema kwa sababu shule nyingi ni kongwe ndio maana miundombinu imeharibika kwa kiasi kikubwa.
“Viongozi wengi tunashinda sana maofisini kuliko kwenda kuyatembelea maeneo yenye changamoto kama hizi za shule za msingi za manispaa ya Iringa kwasababu ukitembelea maeneo yenye changamoto mara kwa mara inakuwa kazi rahisi kuzitafutia ufumbuzi mapema,” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa shule nyingi za msingi manispaa ya Iringa zilijengwa miaka 1980 ndio maana saizi miundombinu imeharibika kutokana na kutokarabatiwa mara kwa mara na kusababisha kuendelea kuharibika kwa kuwa hakuna mikakati ya makusudi ya kukarabati shule hizo.
Kabati aliwaomba wananchi na wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano wa kutosha ilikufanikisha azma ya kuzikarabati shule hizo na kuacha kuangalia Itikadi ya vyama vya siasa kwa kuwa maendeleo hayana siasa.
Naye mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Kibwabwa Isumael Mlenga alimpongeza mbunge huyo kwa kazi anayoifanya ya kusaidia kukarabati shule za msingi za manispaa ya Iringa ni jukumu kubwa analolifanya kwa wanairinga.
“Ni wabunge wachache wenye moyo kama wa Ritta Kabati hivyo tunapaswa kuendelea kumuunga mkono kwenye kazi anazozifanya kwa maendeleo ya watoto wetu wanaosoma katika shule hizo zinazokarabatiwa na mbunge huyo,”alisema Mlenga
Karumerita Mbuta,Zubeiry Mlowela na Romana Lutenga ni wajumbe wa kamati ya shule ya Kibwabwa walimpongeza mbunge huyo kwa ziara zake anazozifanya kuzitambua Changamoto zilizopo mashuleni hasa kwenye shule za msingi hivyo tunaomba ziara zako ziwe na matunda kwa kuboresha miundombinu ya shule ulizotembelea.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MBUNGE VITI MAALUMU IRINGA KUKARABATI SHULE ZA MSINGI ZA MANISPAA YA IRINGA
MBUNGE VITI MAALUMU IRINGA KUKARABATI SHULE ZA MSINGI ZA MANISPAA YA IRINGA
https://4.bp.blogspot.com/-c1Z8Gssrnx0/Wd8rvjKhBXI/AAAAAAAAf9Q/Heq0FqibFqgNRSlDvzRx_lWv5pg054ZJACLcBGAs/s1600/IMG_7345-750x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-c1Z8Gssrnx0/Wd8rvjKhBXI/AAAAAAAAf9Q/Heq0FqibFqgNRSlDvzRx_lWv5pg054ZJACLcBGAs/s72-c/IMG_7345-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/mbunge-viti-maalumu-iringa-kukarabati.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/mbunge-viti-maalumu-iringa-kukarabati.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy