MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191

SHARE:

Kukamilika kwa Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220kV, na usambazaji umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupit...

Kukamilika kwa Mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220kV, na usambazaji umeme vijijini kutoka Makambako-Songea kupitia Njombe, unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa mijini na vijiji vipatavyo 191.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Mradi huo Mhandisi Didas Liyamuya alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari na kusema ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme pia utahusisha upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako cha msongo wa umeme wa kilovolti 220/132/33Kv, na ujenzi wa vituo vingine vipya viwili, vya Madaba na Songea vya msongo umeme wa kilovolti 220/33kV, halikadhalika ujenzi wa mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33 pamoja na kuunganisha wateja 22,700, katika mikoa hiyo.
Akifafanua zaidi, katika mkoa wa Njombe, umeme utasambazwa katika maeneo ya Makambako na viunga vyake, Njombe yenyewe, na Ludewa, wakati mkoa wa Ruvuma umeme utasambazwa katika mji wa Songea na vijiji vilivyo katika wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Madaba, na kuongeza kuwa umeme utakuwa wa msongo wa kilovolti 33 pamoja na ujenzi wa mawasiliano “OPGW”.
“Lengo la mradi huu ambao unafadhiliwa na Serikali ya Swedena kupitia Shirika lake la Misaada ya Kimaendeleo SIDA, Serikali ya Tanzania na Shirika la Umeme Nchini, TANESCO, ni kuboresha hali ya upatikanaji umeme katika maeneo ya uzalishaji na majumbani.” alifafanua.
Wahariri hao walipata fursa ya kutembelea eneo la upanuzi wa kituo cha Makambako ambapo walishuhudia kazi ya kujenga misingi ya mitambo ikiwemo Slope protection. Pia walijionea kazi ya kufunga transfoma kwenye maeneo kadhaa ya Makambako ikiwemo eneo la Lyamkena.
Mhandisi Liyamuya alibainisha kuwa awamu ya kwanza ya mradi wa kusambaza umeme utakamilika Desemba 2017 wakati awamu ya pili utakamilika Novemba 2018.
“Hadi leo hii Oktoba 10, 2017, mradi umekamilika kwa asilimia 63 kwa upande wa mkoa wa Ruvuma na asilimia 39.5 kwa upande wa mkoa wa Njombe na kazi kubwa iliyofanyika ni ubainishaji wa maeneo ya kupitisha laini (njia ya umeme), ubunifu wa jinsi muundo wa njia hiyo utakavyokuwa, ufyekaji wa njia za kupitisha laini, ununuzi wa vifaa pamoja na kusimamisha nguzo za msongo wa 33kV na 400V na kusambaza nyaya, na usimikaji wa Transofa.” alisema.
Hata hivyo Mhandisi Lyamuya alieleza masikitiko yake kwa baadhi ya watu kuchoma moto ovyo misitu ambapo baadhi ya nguzo zilizosimikwa katika kipindi hiki cha mradi zimeungua.
“Nitoe rai kwa watanzania wenzangu, Serikali inafanya juhudi kubwa kuwafikishia huduma hii muhimu ya umeme, na mfahamu kwamba fedha za walipa kodi wa Tanzania Shilingi Bilioni 7 zilitolewa kama fidia, iweje leo tuanze kufanya uharibifu huo.?” Alihoji, na kutaka vimgozi wa serikali kwenye maeneo yote ya mradi kuwahamasisha wananchi kutunza miundombinu hiyo ambayo inaligharimu taifa fedha nyingi.
Na Khalfan Said / K-Vis Blog, Makambako
Meneja wa Mradi huo Mhandisi Didas Liyamuya.
 Mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Lyamkena, mji wa Makambako mkoani Njombe, ambaye ni mteja mpya wa TANESCO, Bw.Thomas Kiwale, (kulia), akihakikiwa wakati wa zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo hilo, na afisa wa TANESCO, Bi.Atuokoe Mhingi.
 Wahariri na mafundi wa TANESCO, wakipita chini ya moja ya transofa zinazoednelea kufungwa kwenye mji wa Makambako.
 Baadhi ya wahariri wakisikiliza maelzo yaliyokuwa yakitolewa na Mhandisi Liyamuya(hayupo pichani), kuhusu utekeelzaji wa mradi huo walipotembelea eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 220kV cha Makambako.
 Baadhi ya wahariri na mafundi wa TANESCO, wakisikiliza maelzo yaliyokuwa yakitolewa na Mhandisi Liyamuya(hayupo pichani), kuhusu utekeelzaji wa mradi huo walipotembelea eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 220kV cha Makambako.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bil Leila Muhaji, akifafanua baadhi ya mambo ambapo alisema, ili kujenga uhusiano mwema na wananchi walio jirani na eneo la Mradi, wateja watatozwa kiasi cha shilingi 27,000 tu kwa kazi hiyo katika kipindi hiki cha utekelezaji wa mradi, na hivyo kuwataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya umeme kwa faida ya taifa na wao wenyewe.
 Atuokoe Mhingi,kutoka TANESCO, akiendelea na zoezi la kuwahakiki wateja walioomba kuunganishiwa umeme kwenye eneo la Lyamkena, Makambako Oktoka 10, 2017.
 Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
Moja ya minara ya kusafirisha umeme wa 220kV. ambao tayari umejengwa nje kidogo ya mji wa Makambako.
 Mhariri wa Mwananchi Online Digital, Peter Nyanje, (kushoto) na Mhariri wa gazeti ka Majira, Bw. Mwafisi wakifurahia jambo.
 Mhariri wa gazeti la Nipashe, Bw. Joseph Mwendapole, (kulia), akionyeshwa moja ya minara ya kupitisha umeme wa 220kV nje kidogo ya Makambako.

 Kazi ya ujenzi wa msingi wa kufunga mitambo kwenye eneo la upanuzi wa kituo cha kupoza umeme wa 220kV Makambako ikiendelea.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Grace Kisyombe wakijadiliana jambo.
 Meneja Mradi wa ujezni wa njia ya kusafirisha umeme kutoka kampuni ya Isolux,Bw.Elmensour,(kulia), akielezea jinsi kazi hiyo inavyoendelea.
Wahariri kutoka kushoto, Peter Nyanje, Joyce Shebe na Nevile Meena.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191
MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA KUNUFAISHA MIJI NA VIJIJI 191
https://2.bp.blogspot.com/-hyS2wn2wKvU/Wd3ixRstVqI/AAAAAAAAfzM/0xWLORCG-b05lSxHm0HigAeNVr7j0mj1gCLcBGAs/s1600/umeme-3-750x375.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-hyS2wn2wKvU/Wd3ixRstVqI/AAAAAAAAfzM/0xWLORCG-b05lSxHm0HigAeNVr7j0mj1gCLcBGAs/s72-c/umeme-3-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/mradi-wa-umeme-wa-makambako-songea.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/mradi-wa-umeme-wa-makambako-songea.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy