NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUTUNGA SHERIA ZINAZOLINGANA KATIKA UDHIBITI WA DAWA

SHARE:

Tanzania imetoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunga sheria zinazolingana ili kuwezesha udhibiti wa pamoja wa d...

Tanzania imetoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunga sheria zinazolingana ili kuwezesha udhibiti wa pamoja wa dawa na vifaa tiba zinazoingia katika nchi wanachama.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya Mpoki ametoa wito huo leo wakati akifungua Kikao cha Siku Mbili cha Kamati ya Maandalizi ya Mpango Ulinganishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Dawa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika katika Hoteli ya New Africa jijiji Dar es Salaam.
“Juhudi za kweli hazina budi kuchukuliwa kudhibiti utengenezaji na uingizaji wa dawa zisizokidhi viwango ambazo mwishowe huwafikia watumiaji na matokeo yake ni wananchi kuathirika kwa kupata madhara makubwa kiafya,”alisema Dk. Mpoki.
Alisisitiza kuwa “magonjwa hayajui mpaka” hivyo uwepo wa dawa zenye ubora unaofanana katika nchi wanachama kunarahisisha matibabu kwa wagonjwa na kunaepusha matumizi ya dawa hafifu katika nchi moja ambako kunakoweza kusababisha usugu wa vidudu vya maradhi.
Dk. Mpoki alieleza wajumbe wa Kamati hiyo ambao ni wawakilishi wa mamlaka za udhibiti wa dawa za nchi wanachama kuwa jukumu na wajibu wa kuhifadhi na kuinua afya ya jamii katika jumuiya lazima zitambuliwe na ziungwe mkono na nchi wanachama kupitia wizara zinazosimamia sekta ya afya.
“Mamlaka hizi zimekuwa kama mlango unaolinda mfumo wa utoaji huduma za afya dhidi ya vifaa tiba na dawa zenye viwango duni, zisizo salama na zisizofanyakazi vyema kuingia katika masoko yetu,” alisema Dk. Mpoki alieleza.
Alibainisha kuwa Tanzania ndio iliyopewa jukumu la kusimamia suala la kanuni hivyo kupitia ufadhili wa washirika mbali mbali wa maendeleo, watalaamu wanaohusika na usalama na dawa na vifaa tiba hukutana mara kwa mara kufanya tathmini kuangalia hatua iliyofikiwa.
“Lengo la Jumuiya ni kuhakikisha kuwa ikifika mwisho wa mwaka huu dawa au kifaa tiba kikiingia katika moja katika nchi zetu kinakuwa na ubora ulio sawa,” alisema Dk. Mpoki.
Katibu Mkuu huyo alieleza pia maazimio ya mkutano huo yatapelekwa, kupitia kwa makatibu wakuu, kwenye Kikao cha Mawaziri wa sekta husika kitakachofanyika nchini Uganda tarehe 23-25 Oktoba mwaka huu.
Mkutano huu ulitanguliwa na mafunzo ya wiki mbili kwa wataalamu wa udhibiti na ukaguzi wa dawa kutoka nchi wanachama ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa pamoja kati ya TFDA na Shule ya Famasi ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya Muhimbili.
Akimkaribisha, Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Bwana Hiiti Sillo aliwashukuru washirika mbalimbali wa Maendeleo ambao wamekuwa wakisaidia programu hiyo ya ulinganishaji kanuni za udhibiti na ukaguzi wa dawa.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUTUNGA SHERIA ZINAZOLINGANA KATIKA UDHIBITI WA DAWA
NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUTUNGA SHERIA ZINAZOLINGANA KATIKA UDHIBITI WA DAWA
https://4.bp.blogspot.com/-y4xT8DroH_4/Wdc9QvMjmUI/AAAAAAAAfiw/FrwyeY_CQ1QyB9nO1kvEbRpW2CEBNuMWQCLcBGAs/s1600/Dkt.-Mpoki-Ulisubisya-750x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-y4xT8DroH_4/Wdc9QvMjmUI/AAAAAAAAfiw/FrwyeY_CQ1QyB9nO1kvEbRpW2CEBNuMWQCLcBGAs/s72-c/Dkt.-Mpoki-Ulisubisya-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/nchi-za-eac-zatakiwa-kutunga-sheria.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/nchi-za-eac-zatakiwa-kutunga-sheria.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy