NITAANZA NA RUSHWA, UZEMBE KATIKA OFISI ZA UMMA – WAZIRI MKUCHIKA

SHARE:

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa atashughulikia suala la rushwa...

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa atashughulikia suala la rushwa pamoja na udanganyifu wa umri unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma hapa nchini.
Mkuchika aliyasema hayo  Jijini Dar es Salaam katika mkabidhiano ya  Ofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki katika ukumbi wa wizara hiyo.
“Tutaongeza kasi ya kurejesha nidhamu, maadili  na mapambano dhidi ya rushwa hapa nchini,” alifafanua waziri Mkuchika
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro pamoja na watumishi wa wizara hiyo, Waziri Mkuchika alisema kuwa atahakikisha anashughulikia suala la watumishi kupandishwa madaraja pamoja na kuongezewa mishahara baada ya kukamilika zoezi la ukaguzi la watumishi hewa.
Aidha alisema kuwa suala la rushwa linatakiwa kujengewa msingi kutoka ngazi ya chini, hivyo ataongea na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ili kuweka somo la rushwa katika mitaala ya elimu hapa nchini kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu.
“Ukienda katika nchi ambazo zimefanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa, mfano Norway, Sweden, pamoja na mataifa ya Scandinavia utakuta wamefanikiwa kwasababu wananchi wote wamepewa elimu dhidi ya rushwa na wanafahamu kwamba rushwa ni adui wa haki, lakini tujiulize watanzania wangapi wanajua kuwa rushwa ni adui wa haki, ni wachache tu,” alisema Waziri Mkuchika.
Aliongeza kuwa, makongamano, semina pamoja na mikutano inayofanya na watumishi wa umma kwa wananchi inapaswa ishirikishe Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) ili kutoa elimu juu ya rushwa na kujenga uelewa  kwa wananchi kwani itasaidia sana kumaliza tatizo la rushwa hapa nchini.
Waziri Mkuchika alimpongeza mtangulizi wake na kuahidi kuendeleza jitihada alizokuwa akiendelea nazo ikiwemo kuondoa watumishi hewa, vyeti feki, wanaoghushi umri  pamoja na uzembe wa wafanyakazi katika ofisi za umma hususani katika Halmashauri.
Kwa upande wake Waziri Kairuki, aliwapongeza watumishi wa Idara, Wakala wa Serikali, Taasisi pamoja na Wizara hiyo  kwa ujumla  kwa ushirikiano na ushauri walioutoa kwa muda aliofanya nao kazi takribani miaka miwili kwa kuimarisha nidhamu, maadili na kuondoa watumishi hewa katika ofisi za umma.
“Tumeweza kurejesha kwa kiasi kikubwa nidhamu katika utumishi wa umma, tumeweza kwa kiasi kikubwa kuanza kujenga misingi ya kuelekea katika kuboresha masilahi ya watumishi umma maana ilikuwa ni lazima tuanze kusafisha kwanza lakini pia tumeweza kuondoa watumishi hewa, pamoja na kuondoa watu ambao hawakuwa na sifa stahiki katika utumishi wa umma,” alifafanua Waziri Kairuki.
Waziri Mkuchika aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufuatia mabadiliko yaliyofanywa katika baraza la mawaziri na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo aliyekuwa anaongoza wizara hiyo Angelah Kairuki aliteuliwa kuwa waziri wa madini.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NITAANZA NA RUSHWA, UZEMBE KATIKA OFISI ZA UMMA – WAZIRI MKUCHIKA
NITAANZA NA RUSHWA, UZEMBE KATIKA OFISI ZA UMMA – WAZIRI MKUCHIKA
https://3.bp.blogspot.com/-wSsHamTzobI/Wd8swKh0YpI/AAAAAAAAf9g/TnYE31ShjWgflqoH-8LheD2gXI92bXa9ACLcBGAs/s1600/0-6-750x375.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-wSsHamTzobI/Wd8swKh0YpI/AAAAAAAAf9g/TnYE31ShjWgflqoH-8LheD2gXI92bXa9ACLcBGAs/s72-c/0-6-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/nitaanza-na-rushwa-uzembe-katika-ofisi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/nitaanza-na-rushwa-uzembe-katika-ofisi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy