TAMKO LA WIZARA YA AFYA KATIKA SIKU YA AFYA YA AKILI LEO OKTOBA 10

SHARE:

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY MWALIMU (MB) KUHUSU SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI TAREHE 1...

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE. UMMY MWALIMU (MB) KUHUSU SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI TAREHE 10 OKTOBA 2017
Ndugu Wananchi,
Siku ya Afya ya Akili Duniani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 10 ya Mwezi Oktoba.
Kaulimbiu  ya  Maadhimisho ya  Siku ya  Afya ya Akili Duniani mwaka 2017 ni “Afya ya Akili Mahali pa Kazi” Kauli mbiu hii  inalenga kuhamasisha Waajiri na watunga sera namna bora ya kuhusisha Afya ya Akili katika ngazi mbalimbali za kutengeneza miongozo ya kisera na kuifanya afya bora ya akili kuwa ni sehemu ya ustawi wa wafanyakazi.
Ndugu Wananchi,
Tanzania kama ilivyo nchi zingine wanachama wa shirika la Afya Duniani wanaadhimisha siku hii, ambapo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa shughuli mbalimbali za kutoa elimu kuhusu umuhimu wa afya ya akili  mahali pa kazi na kuwafanya waajiri na wafanyakazi kutambua umuhimu wa afya bora ya kiakili na  huduma za  afya ya akili.
Ndugu Wananchi,
Tunapozungumzia afya tunamaanisha hali ya ustawi wa mwanadamu kimwili, kiakili na kijamii. Mtu mwenye afya njema ya akili anaaminika kwa kutengemaa katika namna anavyofikiri, anavyohisi, na anavyotambua mambo, ambayo kwa pamoja hujionyesha katika matendo yake ya kila siku ikiwa ni pamoja na jinsi anavyohusiana na kushirikiana na wenzake katika familia na jamii  na mahali pa kazi kwa ujumla.
Magonjwa ya akili ni magonjwa ambayo yanaathiri au yanapelekea mabadiliko katika kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda, na hivyo kuwa na mabadiliko ya kitabia au mwenendo uliotofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila, desturi, na nyanja nyingine za kijamii. Tabia hizo zinatokana na ugonjwa wa akili kuathiri ufanisi na shughuli za mtu husika (mgonjwa) pamoja na kuathiri uhusiano wake katika jamii na hivyo huathiri jamii nzima inayomzunguka.
Visababishi vya magonjwa ya akili vimegawanyika katika sababu za kibaolojia, kisaikolojia na kijamii na mjumuiko  wa visababishi hivi ndivyo vinavyopelekea mtu kuwa na dalili  za ugonjwa wa akili.
Ndugu Wananchi,
Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha kuwa kati ya watu wazima wanne mmoja kati yao alishapata au alishaona mtu mwenye matatizo ya kiakili, ambayo hutokana na mila na desturi zilizopitwa na wakati, unyanyasaji, unyanyapaa na kutengwa au kubaguliwa kwa namna yeyote.
Hali kadhalika hata katika nchi yetu tumekuwa tukikabiliwa na matatizo kama hayo ya mila na desturi zisizo rafiki, unyanyapaa na ubaguzi ambao unasababisha pia ufinyu wa bajeti, uhaba wa wataalamu katika vituo vya kutolea huduma, uhaba wa vifaa tiba na dawa kwa wagonjwa wenye matatizo ya kiakili, kijamii na kisaikolojia. Tunapaswa kukumbuka kuwa hakuna afya njema ya kimwili kama hakuna afya ya akili; na pia nchi yetu ikiwa na wafanyakazi wenye afya bora ya akili ni hazina kubwa kwa Taifa letu.
Ndugu Wananchi,
Katika kukabiliana na ukweli huu jitihada mbalimbali zimefanywa za kutoa huduma za afya ya akili ikiwa ni pamoja na kutengeza Mwongozo wa kisera wa afya ya akili ya mwaka, 2006 na Sheria ya Afya ya Akili ya mwaka 2008 ambavyo unatoa mwongozo wa namna ya kutoa huduma. Aidha, serikali inaendelea kuhamasisha waajiri kuwekea mkazo mambo mbalimbali ya kuimarisha huduma za afya ya akili katika mipango yao, na kuhakikisha kila Mkoa unaimarisha huduma hizi katika ngazi ya Mikoa yote Tanzania Bara.
Vilevile serikali inaendelea kuwajengea uwezo watoa huduma za afya ya akili nchini ili waweze kutambua na kubaini mapema dalili za magonjwa ya akili na kutoa matibabu stahiki au rufaa kwa wakati muafaka. Pia, tumeimarisha matibabu ya magonjwa ya akili na saikolojia katika hospitali za mikoa na rufaa hii ikiwa ni pamoja na kupeleka wataalamu wa afya ya akili wakiwepo madaktari bingwa na wauguzi bingwa ili kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje na wale wa ndani/ waliolazwa.
Ndugu Wananchi,
Watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo kuhusu magonjwa ya akili, na kufikia hatua ya kuhusisha na laana, kurogwa, kuwa na mapepo au kutupiwa majini; Magonjwa ya akili ni magonjwa kama yalivyo mengine na yanaweza kumtokea mtu yeyote wa rika lolote na muda wowote, hivyo basi wananchi, wanafamilia na jamii kwa ujumla tunapaswa kujua na kutambua dalili za magonjwa ya akili na kuwasaidia kupata matibabu, kupunguza unyanyasaji, unyanyapaa na kuwatenga wagonjwa wa akili. Taarifa ya afya na magonjwa ya akili ya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa takribani wagonjwa 611,789 wameweza kuhudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya nchini.
Katika kukabiliana na wimbi la ugonjwa wa Afya ya akili wataalamu na waajiri wataendelea kuelimisha jamii juu ya magonjwa ya akili na kupinga vitendo vya unyanyasaji, unyanyapaa na kuwatenga wagonjwa hivyo, kuwawezesha kufikishwa maeneo ya utolewaji wa huduma na tiba mapema ili wasaidiwe kama walivyo wagonjwa wengine.
Ndugu Wananchi,
Dhamira kuu ya maadhimisho ya mwaka huu 2017, ni kuhakikisha afya ya akili inakuwa sehemu ya agenda kila mwaka mahali pa kazi na kwamba waajiri na waajiriwa waweze kuweka mikakati/mipango ambayo itazuia/ itapunguza au kuondoa visababishi vya magonjwa ya akili na uwezeshaji wa utambuzi wa mapema kwa walio na dalili za magonjwa ya akili na hivyo kupatiwa tiba.
Aidha, dhamira pia inalenga kuhakikisha kuwa mahali pa kazi ni mahala salama na pasipokuwa na visababishi/vichochea/vihatarishi vinavyopelekea waajiri na waajiriwa kupata dalili za magonjwa ya akili kwa sababu ndio sehemu ambayo mwajiriwa/waajiriwa wanakaa muda mrefu kuliko muda wa majumbani.
Vilevile, dhamira inalenga  kuongeza thamani, heshima na utu wa mgonjwa wa akili, kuzifanya  huduma za afya ya akili kama sehemu muhimu ya huduma ya mwili wa binadamu, kupunguza unyanyapaa, kutengwa na kunyanyaswa, kuifanya jamii kuongeza uelewa na kutambua magonjwa ya akili kama magonjwa mengine na hivyo kuyapa kipaumbele.
Ndugu Wananchi,
Serikali imeendelea na utekelezaji wa Sera ya Afya ya mwaka (2007) ambayo inalenga kutoa huduma bila malipo kwa wagonjwa wa akili na magonjwa mengine yasiyoambukiza.
Aidha Sera ya Mwongozo wa Huduma za Afya ya Akili inasisitiza utoaji wa huduma za Afya ya Akili bila malipo.  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kutambua uwepo wa maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili duniani kama sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani.
Ndugu Wananchi,
Ili kuboresha hali ya afya ya akili Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kwamba: – inaongeza uelewa wa jamii kuhusu visababishi, dalili na huduma zinazohusiana na afya na magonjwa ya akili ikiwemo:
  • Watumishi wa afya wanapatiwa mafunzo maalum ya namna ya kuchujua/kuchunguza dalili za magonjwa ya akili na kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa wa akili.
  • Kufanya tafiti mbalimbali zinazosaidia kuboresha huduma za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya akili katika jamii.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TAMKO LA WIZARA YA AFYA KATIKA SIKU YA AFYA YA AKILI LEO OKTOBA 10
TAMKO LA WIZARA YA AFYA KATIKA SIKU YA AFYA YA AKILI LEO OKTOBA 10
https://2.bp.blogspot.com/-8-1Mfg95AS0/WdzvWejDJkI/AAAAAAAAfto/50PFqvmrGoEl9wUXOcu1yLOz1dvpbQ_7ACLcBGAs/s1600/xPICHA-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.UOC6h7t0sb.webp
https://2.bp.blogspot.com/-8-1Mfg95AS0/WdzvWejDJkI/AAAAAAAAfto/50PFqvmrGoEl9wUXOcu1yLOz1dvpbQ_7ACLcBGAs/s72-c/xPICHA-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.UOC6h7t0sb.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/tamko-la-wizara-ya-afya-katika-siku-ya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/tamko-la-wizara-ya-afya-katika-siku-ya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy