TANGA CEMENT YATOA MIFUKO 1,000 YA SARUJI KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI

SHARE:

Jeshi la Polisi mkoani hapa, limepokea jumla ya tani hamsini sawa na mifuko elfu moja ya Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na...

Jeshi la Polisi mkoani hapa, limepokea jumla ya tani hamsini sawa na mifuko elfu moja ya Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na Mbili na Laki Tano toka kampuni ya Saruji yaTanga (Tanga Cement) ili ziweze kusaidia ujenzi wa nyumba za Askari wa Jeshi hilo ambalo hivi karibuni walipatwa na majanga ya moto yaliyosababisha nyumba za familia 13 kuungua na kuteketeza karibu kila kitu. 
 
Akipokea shehena hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo aliishukuru Kampuni ya Tanga Cement kwa kujitoa na kutambua mchango wa askari katika kuimarisha  usalama, na kuahidi kusimamia ili ujenzi huo kasi yake iongezeke.
 
Alisema mbali na Kampuni hiyo pia aliwaomba watu wengine binafsi pamoja na Makapuni mengine waige mfano toka kwa kampuni hiyo kuisaidia jamii hasa katika sekta mbalimbali kama vile elimu, afya  na majanga kama haya.
 
Kamanda Mkumbo pia alitumia fursa hiyo kushukuru watu binafsi , makampuni, taasisi pamoja na majeshi ya Ulinzi na Usalama kama vile Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi Kilimanjaro, Chuo cha Polisi Moshi na Jeshi la Magereza.
 
Wengine ni kiwanda cha Magodoro cha Tanfoam, kiwanda cha A to Z, Ofisi ya Mwanasheria mkoani hapa, Green Valley School na Kampuni ya Otterlo Business Corporation Ltd (OBC) pamoja na watu binafsi ambao walitoa msaada wa fedha, Chakula, Saruji nguo pamoja na Magodoro.
 
Kwa upande wake Meneja Biashara wa kampuni hiyo Bw. Peet Brits alisema kwamba, wao kama kampuni wameweka mkazo kusaidia katika elimu, afya, maendeleo ya Jamii pamoja na mazingira lakini kwenye majanga mbalimbali kama vile ajali za moto.
 
Alisema kwamba anafahamu kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi katika kudumisha usalama ambapo unasaidia kuvutia mazingira mazuri ya kibiashara hapa nchini. Alisema wametoa msaada huo ili usaidie kujenga makazi ya familia za askari.
 
Bw. Brits alisema anajua walichochangia hakiwezi kutosheleza  lakini wanaamini kitasaidia kwenye ujenzi wa nyumba hizo na kuzitaka kampuni pamoja na taasisi kusaidia Jeshi la Polisi ambalo linaimarisha usalama hali ambayo inasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.
 
Familia 13 za Jeshi hilo mkoani hapa zilikosa makazi siku ya tarehe 27/09/2017 baada ya nyumba zao zilizopo katika moja ya Kambi za Polisi kuungua kwa moto uliotokana na hitilafu ya umeme ulitokea muda wa saa 12:45 jioni.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TANGA CEMENT YATOA MIFUKO 1,000 YA SARUJI KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI
TANGA CEMENT YATOA MIFUKO 1,000 YA SARUJI KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI
https://4.bp.blogspot.com/-kSS0qMcexPs/WdzrG8Ps-4I/AAAAAAAAftM/ftzYFulN1yEWxOsEbkICcv3YdwQILYYhACLcBGAs/s1600/JC9A6369-750x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-kSS0qMcexPs/WdzrG8Ps-4I/AAAAAAAAftM/ftzYFulN1yEWxOsEbkICcv3YdwQILYYhACLcBGAs/s72-c/JC9A6369-750x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/tanga-cement-yatoa-mifuko-1000-ya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/tanga-cement-yatoa-mifuko-1000-ya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy