TEMESA YATAKIWA KUKUSANYA MADENI YAKE YOTE KWA WADAIWA

SHARE:

Na Thobias Robert Naibu Waziri wa Ujenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa ameitaka Wakala wa Ufundi na...

Na Thobias Robert
Naibu Waziri wa Ujenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa ameitaka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kukusanya na kutumia madeni zaidi ya bilioni 10, inayozidai  taasisi, idara na wakala mbalimbali wa sekta za umma na binafsi ili watumie pesa hizo katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.
Waziri ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi kuongea na kuangalia  utendaji kazi wa wafanyakazi pamoja na kukagua  mitambo inayotumiwa na wakala hiyo iliyo chini ya wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.
“Madeni ni rasilimali ambayo tunahitaji kuisimamia vyema, chambueni vizuri  madeni ambayo taasisi inadai kwenye taasisi, idara na wakala mbalimbali za serikali ili tuweze kuona namna gani tutafanya ili madeni hayo yalipwe, kwa sababu tukikaa na madeni mengi yatatukwamisha katika shughuli zetu,” alisisitiza Waziri Kwandikwa.
Aidha alisema kuwa wakala na idara zinazofanya kazi na TEMESA zinapaswa kulipa madeni wanayodaiwa ili kuiwezesha taasisi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kutumia vifaa na miundombinu ya kisasa inayoandana na utoaji wa huduma unaofanya na TEMESA.
“Nitoe wito kwa taasisi mbalimbali zinazodaiwa na TEMESA ziweze kulipa haraka hayo madeni ili tuweze kufanya kazi vizuri zaidi, maana wangekuwa wanakwenda kwenye kampuni binafsi  kama wanadaiwa basi magari yao yangekuwa yanakamatwa, sasa isije tukafika wakati na sisi kuanza kampeni ya kuzuia magari, kwa sababu lazima TEMESA isimame ili tuweze kutoa huduma vizuri,” aliongeza Waziri Kwandikwa.
Aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma, uzalendo, umoja na kuzingatia sheria, taratibu pamoja na kanuni zilizowekwa kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja na wadau wanaotumia taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Ngwatu alisema kuwa wamefanikiwa kufanya mambo mbalimbali tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani ambapo, wameweza kununua boti ndogo 4 kwa ajili ya matumizi ya dharura katika maeneo mbalimbali katika mikoa ya Mtwara na Tanga.
“Katika mwaka wa fedha 2016/2017, ujenzi wa kivuko cha Mv. Magogoni umekamilika kwa gharama ya shilingi bilion 7, kivuko cha MV. Tanga  kimekamilika kwa gharama ya shilingi bilioni 4, pia kivuko cha Mv Pangani kimekarabatiwa”.alifafanua  Dkt. Ngwatu.
Aliongeza kuwa, mwaka huu wa fedha TEMESA wana mpango wa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maegesho ya kivuko cha Chato, mkoani Geita, ujenzi wa maegesho ya Lindi-Kitunda na0 ununuzi wa kivuko kipya cha Kigongo Busisi katika ziwa Viktoria kwa gharama ya bilioni 8.9 ambao utakamilika mwezi Januari mwakani.
Vilevile TEMESA inatarajia kufanya ununuzi wa kivuko kipya cha Kayenze-Bezi mkoani Mwanza, kukarabati vivuko vya Misungwi na Sengerema vilivyopo ziwa viktoria, pamoja na kivuko cha Kigamboni, ujenzi wa maegesho ya Malinyi pamoja na kuweka mashine za ukataji  tiketi kwa njia ya kielektroniki katika kivuko cha Magogoni-Kigamboni.
Aidha Dkt. Ngwatu alisema kuwa TEMESA wanatarajia kuzalisha zaidi ya shilingi bilioni 71 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/18, ambapo zaidi ya bilioni 40.3 ya fedha hizo ni kutoka katika vyanzo vya ndani na bilioni 22.7 ni fedha za ruzuku kutoka serikalini.
Aidha Dkt. Ngwatu alisema kuwa, kwa mwaka, wa fedha 2017/2018, wakala unatarajia kukusanya  zaidi ya shilingi bilioni 71 ambapo zaidi ya billion 40.3 ni kutoka katika vyanzo vya ndani na zaidi ya shilingi bilioni 22.7 ni fedha za ruzuku kutoka serikalini.
TEMESA ni wakala wa ufundi na umeme iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambayo ilianzishwa mwaka 1997 kwa lengo la kutoa huduma za uhandisi wa mitambo na umeme katika taasisi za serikali na binafsi.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TEMESA YATAKIWA KUKUSANYA MADENI YAKE YOTE KWA WADAIWA
TEMESA YATAKIWA KUKUSANYA MADENI YAKE YOTE KWA WADAIWA
https://4.bp.blogspot.com/-6OABbfokyWw/Wd--faaLW4I/AAAAAAAAgCI/46nSpgjTIhYAkr2mHrOclpLpe4l1HVJfwCLcBGAs/s1600/xNew-Picture-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.7Dx-RuTQ86.webp
https://4.bp.blogspot.com/-6OABbfokyWw/Wd--faaLW4I/AAAAAAAAgCI/46nSpgjTIhYAkr2mHrOclpLpe4l1HVJfwCLcBGAs/s72-c/xNew-Picture-3-750x375.jpg.pagespeed.ic.7Dx-RuTQ86.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/temesa-yatakiwa-kukusanya-madeni-yake.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/temesa-yatakiwa-kukusanya-madeni-yake.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy