WANAFUNZI WA CHUO CHA ARDHI TABORA WAMLILIA NAIBU WAZIRI WA ARDHI

SHARE:

Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wamekutana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla na kumuomba a...

Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wamekutana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla na kumuomba atatue changamoto zinazowakabili.
Changamoto kubwa zilizoibuliwa na Wanafunzi hao ni suala la upatikanaji wa vifaa vya upimaji ardhi, uandaaji na uchoraji ramani, mafunzo ya vitendo, malazi na suala la uhakika wa ajira baada ya kumaliza  masomo yao.
Wanafunzi hao walimueleza Mhe. Mabula adha wanayoipata katika kujifunza hasa wakati vinapohitajika vifaa vya upimaji na uandaaji ramani ambavyo kwa chuo hicho ni vichache na vina gharama kubwa kwao kuvimudu.
Katika kujibu hoja hizo Mhe. Mabulla alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Tabora Bibi Queen Mwashinga na kumuagiza Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Bwana Biseko Musiba kuwatumia wanafunzi hao katika kuupanga mji wa Tabora na miji ya jirani na hasa katika katika kutatua migogoro ya ardhi.
Kuhusu vifaa vya upimaji ardhi, uandaaji na uchoraji ramani Mhe Mabulla alitembelea mitambo mipya ya uandaaji ramani ambayo kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo imegharimu zaidi ya milioni 200 na ipo tayari kutumiwa na wanafunzi hao katika kujifunza.
Mkuu wa chuo hicho ameeleza kwamba vifaa hivyo vitatumiwa na wanafunzi hao katika mafunzo kwa vitendo na hata kutumika katika kuchora, kuandaa na kuchapisha ramani na machapisho mengine yenye ubora wa kutosha.
Kuhusu suala la ajira Naibu Waziri huyo aliwaambia wanafunzi hao kwa sasa serikali ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli imejipanga kutatua migogoro ya ardhi na kuboresha taaluma ya ardhi, mipango miji, upimaji na ramani hivyo baada ya zoezi la uhakiki Serikali itaajiri maafisa hao kwa wingi. Hata hivyo wanafunzi hao wataendelea kutumiwa katika shughuli mbalimbali za upangaji mji wakati wakiwa chuoni kwa malipo maalumu.
Na katika hatua nyingine Mhe. Mabula ameliagiza Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) mkoani tabora kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Mji wa Tabora kujenga mabweni ya wanafunzi hao, nyumba za wafanyakazi na ofisi katika eneo linalomilikiwa na Chuo cha Tabora kwa kuzingatia mpango kabambe wa mji huo.
Kuhusu suala la kushughulikia migogoro iliyopo mkoani Tabora Mhe. Mabula ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanamaliza tatizo la uvamizi wa Viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na vile vinavyomilikiwa na Taasisi nyingine na watu binafsi ili waweze kuviendeleza.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara hiyo ya siku moja katika Chuo cha Ardhi Tabora.
Alisema kuwa ni vema Halmashauri zote zikahakikishe zinaondoa migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha watu wenye maeneo yao ambayo yamevamiwa au kugawia watu wengine ambao sio wamiliki kihalali wanawaondoa na kuwarejeshea watu au Taasisi ambazo ndio zinazomiliki maeneo husika.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla  akiteta na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla  akiongea na wanafunzi na viongozi wa Chuo cha Ardhi Tabora.
Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wakimkisikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla alipokuwa akiwafafanulia jambo
Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wakimkisikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla alipokuwa akiwafafanulia jambo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akikagua vifaa vya uchapaji na uandaaji wa ramani vya Chuo cha Ardhi Tabora vilivyogharimu kiasi cha milioni 200.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akikagua vifaa vya uchapaji na uandaaji wa ramani vya Chuo cha Ardhi Tabora vilivyogharimu kiasi cha milioni 200.
Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Bwana Biseko Musiba akimuonesha mandhari ya Chuo cha Ardhi Tabora Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WANAFUNZI WA CHUO CHA ARDHI TABORA WAMLILIA NAIBU WAZIRI WA ARDHI
WANAFUNZI WA CHUO CHA ARDHI TABORA WAMLILIA NAIBU WAZIRI WA ARDHI
https://1.bp.blogspot.com/-3aJcyGKZbT8/Wd9rxuGANvI/AAAAAAAAgAA/LquxxQsyM1oMpMa14c80NjY00N_5hfwfwCLcBGAs/s320/x11-6-750x375.jpg.pagespeed.ic.cXqw627FZO.webp
https://1.bp.blogspot.com/-3aJcyGKZbT8/Wd9rxuGANvI/AAAAAAAAgAA/LquxxQsyM1oMpMa14c80NjY00N_5hfwfwCLcBGAs/s72-c/x11-6-750x375.jpg.pagespeed.ic.cXqw627FZO.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/wanafunzi-wa-chuo-cha-ardhi-tabora.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/wanafunzi-wa-chuo-cha-ardhi-tabora.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy