WAZIRI KIGWANGALLA ATANGAZA VITA DHIDI YA MAJANGILI

SHARE:

Muda mfupi baada ya kula kiapo, Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, ametoa onyo kali kwa majingili nchini na kuwa...

Muda mfupi baada ya kula kiapo, Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, ametoa onyo kali kwa majingili nchini na kuwataka kuacha mara moja vitendo hivyo kwani amejipanga kuhakikisha anatokomeza vitendo hivyo.
Dkt. Kigwangalla ametoa onyo hilo leo Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa mawaziri na naibu mawaziri.
“Majangili waanze kukimbia wenyewe pale wanapowaona wanyama kwani tutawashughulikia ipasavyo na kuhakikisha tunakomeza vitendo hivi viovu katika nchi yetu,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Kuhusu utalii, Dkt. Kigwangalla amesema kuwa watalii wamekuwa wakiongezeka lakini si kwa kiwango cha kuridhisha hivyo Serikali itafanya juhudi za makusudi kutangaza vivutio vya utalii kwa njia za kisasa ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa ubunifu katika kujitangaza itabidi utumike ili kuhakikisha Tanzania inavutia watalii wengi kutoka nje hususani soko jipya la China na nchi nyingine ikiwemo Marekani na nchi za Ulaya.
Kwa kufanya hivyo pato la Taifa kutokana na utalii litaongezeka kuliko ilivyo sasa, alisema Kigwangalla.
Aidha, Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amesema atashirikiana na wizara nyingine kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji ili lipatikane suluhisho la kudumu.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo, amesema atahakikisha watumishi wa umma katika wizara yake wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea.
Kwa mujibu wa Jafo, uadilifu, uwajibika na nidhamu ni mambo ambayo yatatiliwa mkazo katika wizara yake ili kuwa na utumishi wenye tija.
Amewataka wakuu wa mikoa, wilaya kufanya kazi kwa mashindano ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo katika sehemu husika na kuchochea ukuaji wa uchumi hasa wa viwanda.
“Wakuu wa mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri muwe vinara katika utendaji wenu mkiwasimamia walioko chini yenu kwa weledi ili muweze kwenda na spidi ya Serikali ya Awamu ya Tano,” alisema Jafo.
Naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akizungumza baada ya kuapishwa amesema atahakikisha sekta ya habari inapewa kipaumbele kwani habari ni jambo muhimu katika suala zima la mawasiliano.
Shonza atahakikisha weledi katika sekata ya habari unazidi kuimarishwa ilikuondoa upotoshwaji ambao umekuwa ukijitokeza katika baadhi ya vyombo habari.
Kuhusu upatikanaji wa habari kwa sehemu kubwa ya watanzania, Shonza amesema atajitahidi kufanya habari ziwafakie watanzania wengi zaidi ili kujenga jamii yenye ufahamu wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yao.
Katika hafla hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha jumla ya Mawaziri nane na Manaibu Mawaziri 16 ambao wameanza kazi mara baada ya kuapishwa kwa kuhudhuria kikao cha Maalum cha Baraza la Mawaziri.
Baadhi ya mawaziri waliokula kiapo leo ni Mhe. Angella Kairuki (Madini), Mhe. George Mkuchika (Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Mhe. Hamis Kigwangwalla (Maliasili na Utalii) na Suleiman Jafo (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa).
Kwa upande wa Manaibu Mawaziri, Mhe. Rais amewaapisha jumla 16 ambao baadhi yao ni Mhe. Stella Manyanya (Naibu waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji), Mhe. William Ole Nasha (Elimu, Sayansi na Teknolojia), Dkt. Faustine Ndungulile (Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), Mhe. Stella Ikupa (Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemeva) na Mhe. Juliana Shonza (Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo).

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAZIRI KIGWANGALLA ATANGAZA VITA DHIDI YA MAJANGILI
WAZIRI KIGWANGALLA ATANGAZA VITA DHIDI YA MAJANGILI
https://3.bp.blogspot.com/-O0LYjWO5reQ/WdxoGXR93JI/AAAAAAAAfsQ/3IEcVL9Fao0XPeDyed597Lmx37ntg9JJQCLcBGAs/s1600/DSC_1230-1-702x375%2B%25281%2529.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-O0LYjWO5reQ/WdxoGXR93JI/AAAAAAAAfsQ/3IEcVL9Fao0XPeDyed597Lmx37ntg9JJQCLcBGAs/s72-c/DSC_1230-1-702x375%2B%25281%2529.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/waziri-kigwangalla-atangaza-vita-dhidi.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/waziri-kigwangalla-atangaza-vita-dhidi.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy