WAZIRI MWAKYEMBE AAHIDI KUWATOKOMEZA WAHARAMIA WA KAZI ZA FILAMU

SHARE:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kuhakikisha kwamba suala la uharamia wa kazi za fila...

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kuhakikisha kwamba suala la uharamia wa kazi za filamu za Watanzania nchini unakomeshwa mara moja kwa kuwasaka wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.
Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wamiliki wa Majumba ya Kuonyeshea Sinema ambapo moja ya changamoto kubwa aliyotajiwa na wamiliki hao ni suala la uharamia wa kazi za sanaa jambo ambalo linawakwamisha wamiliki hao kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa wakivujisha filamu mpya kwa kuziuza kiholela mitaani na wengine wakihuisha filamu hizo katika mitandao ya kijamii jambo linalosabibisha hasara kubwa kwa wasanii na wamiliki wa majumba ya sinema.
Mhe. Mwakyembe amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu hao wanaojihusisha na uharamia wa kazi za filamu za Watanzania huku akiapa kuwashughulikia popote walipo watu hao ili kuhakikisha kuwa Wasanii wananufaika na kazi zao na pia Wamiliki wa Majengo ya Sinema wananufaika pia kwa kuonyesha kazi za wasanii hao kwa utaratibu ambao hautomuumiza msanii mwenye kazi yake.
“Najua baadhi ya Wamiliki wa Majumba ya Sinema mnapata hasara, na hata baadhi ya Wasanii pia, suala hili linanikera sana na kamwe haikubaliki hata kidogo, tutahakikisha kwamba watu wa namna hii wanatoweka katika tasnia yetu, tutawasaka popote walipo na kuwapeleka kwenye vyombo vya Sheria kwani Serikali hii sio ye mchezo na watu wa namna hii,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, yeye kama Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo atahakikisha kwamba hamasa ya kutosha inatolewa kwa Watanzania ili wawe na utamaduni wa kuangalia sinema zinazotengenezwa nchini katika Majumba ya Sinema yaliyopo nchini.
Aidha, Dkt. Mwakyembe amewapongeza Wasanii nchini kwa kutoa kazi nyingi huku akiwataka kuhakikisha kwamba ubora unazingatiwa na maadili yanazingatiwa kwa ajili ya jamii na pia amewashauri Wamiliki wa Majumba hayo kutenga siku maalum ambayo itakuwa ikitumika kuonyesha Sinema za Kiswahili zenye maadili na kuzitaka sinema hizo kupewa muda wa kutangazwa katika vyombo vya habari nchini ili wananchi wengi wapate kuzijua na kuweza kutembelea majumba hayo kwa ajili ya kuzitazama.
“Mi nadhani na sisi Tanzania tukianzisha utamaduni wa kwamba siku Fulani ni siku ya kuonyesha Sinema za Kiswahili tu, hii itaweka historia nchini lakini iwe picha nzuri tu na tuzitangaze filamu hizo na sisi kama Wizara tuna haja ya kuongea na baadhi ya vituo vya televisheni, magazeti pamoja na redio kuzitangaza filamu hizo kwani hii itasaidia kuinua soko la filamu nchini. Bodi ya Filamu Tanzania hakikisheni kwamba pindi itakapoamuliwa kuwa siku fulani ni siku ya kuonyesha filamu za Kiswahili basi muone haja ya kuzipunguzia tozo baadhi ya filamu hizo zitakazokuwa zikionyeshwa lakini tu mpaka hapo itakapoamuriwa,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Juliana Shonza amewapongeza Wasanii wa Tanzania kwa kujitoa kwao katika kuonyesha vipaji vyao katika kuhakikisha kwamba vipaji hivyo vinaitangaza Tanzania Kimataifa.
“Nafurahi kuona kuwa Filamu za Watanzania zinafanya vizuri na Tanzania tuna Waigizaji wanaofanya vizuri kwahiyo naamini kwamba mkiitumia vizuri hiyo fursa ya uigizaji mtakuwa mnaitendea haki nchini yetu na kuinua vipaji vyenu lakini pia mtakuwa mmeitangaza Tanzania Kimataifa,” alisema Mhe. Shonza.
Mhe. Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Naibu wake Mhe. Juliana Shonza kwa pamoja wamekuwa wakikutana na wadau mbalimbali wa kisekta ikiwa ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea lengo likiwa kutambua changamoto zao na namna ya kuzitatua kwa manufaa ya Taifa.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAZIRI MWAKYEMBE AAHIDI KUWATOKOMEZA WAHARAMIA WA KAZI ZA FILAMU
WAZIRI MWAKYEMBE AAHIDI KUWATOKOMEZA WAHARAMIA WA KAZI ZA FILAMU
https://4.bp.blogspot.com/-kBGqWKgF5iA/Wd8sFXyZVmI/AAAAAAAAf9U/AluxqK1wg1oLwyZTHdYVh8XkCYXiV5zVQCLcBGAs/s1600/unnamed-28-702x375.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-kBGqWKgF5iA/Wd8sFXyZVmI/AAAAAAAAf9U/AluxqK1wg1oLwyZTHdYVh8XkCYXiV5zVQCLcBGAs/s72-c/unnamed-28-702x375.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/waziri-mwakyembe-aahidi-kuwatokomeza.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/waziri-mwakyembe-aahidi-kuwatokomeza.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy