WIZARA YA AFYA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUFIKIA 2020

SHARE:

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali  ha...

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali  hawapo pichani wa Wizara ya afya kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini  leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Wakati wa kikao chake na wakuu hao.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto Dkt.  Faustine Ndungulile wa kwanza kushoto akiongea na wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya hawapo pichani kuhusiana na kuimarisha huduma bora za afya nchini  leo jijini Dar es salaam, katikati ni Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu na kulia ni Katibu Mkuu Wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya. Alipokutana na wakuu hao.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo  Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakimpongeza Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndungulile hayupo pichani mara baada ya kuwapa maelezo wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Wizara ya afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Waziri mwenye dhamani hiyo  Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile hawapo pichani wakati wa kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akiteta jambo na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile kushoto mara baada ya  kikao na wakuu wa idara hizo leo jijini Dar es salaam.
………………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WIZARA ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto imejidhatiti kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mpaka kufikia 2020 ili kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga .
Hayo yamesemwa na Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokutana na Wakuu wa Idara na vitengo Mbalimbali kwa ajili ya utambulisho wa Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile  katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
“Vifo vya wajawazito vimekua tishio nchini hivyo ni lazima tuimarishe huduma za afya ya mama na mtoto ili tufikie malengo ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi mpaka kufikia 2020 ili kujenga taifa lenye watu wenye afya bora” alisema Waziri ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika kuboresha hilo amewaagiza wakuu wa idara wizara ya afya kushirikiana na mfuko wa bima ya afya nchini(NHIF) kuona kama kuna uwezekano wa kuanzisha bima ya afya kwa wajawazito kwa bei nafuu hadi kufikia Julai mosi 2018.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa wanamipangilio ya kutokomeza kabisa tatizo la dawa nchini kwa kuweka mpango mkakati kati ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na vituo  vitoavyo huduma za afya  ili kuepuka tatizo hilo lisijirudie mara kwa mara .
Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndungulile amesema kuwa ameshukuru kwa kupewa dhamana hiyo na atashirikiana vyema na Waziri pamoja na watendaji wa Wizara hiyo ili kuleta ufanisi na Huduma bora za afya nchini.
“Nitashirikiana na Waziri wangu pamoja na nyinyi watendaji wenzangu katika kusimamia na kutekeleza sera ya afya ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa watanzania wote bila ya kujali rika,jinsia wala umri” alisema Dkt. Ndungulile

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa wamepokea maagizo hayo amabayo baadhi  wameanza kuyatekeleza na mengine  atawahimiza watendaji wake kuendana na kasi ya awamu ya tano ya HAPA KAZI TU ili kuifikisha nchi katika afya bora.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WIZARA YA AFYA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUFIKIA 2020
WIZARA YA AFYA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO KUFIKIA 2020
https://4.bp.blogspot.com/-6CmrrG5EPZw/WeDUH1bZpTI/AAAAAAAAgNY/RlryMM9CFkAwiNi8HRGc6EB4vAhiqrP0ACLcBGAs/s1600/1-66.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-6CmrrG5EPZw/WeDUH1bZpTI/AAAAAAAAgNY/RlryMM9CFkAwiNi8HRGc6EB4vAhiqrP0ACLcBGAs/s72-c/1-66.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/10/wizara-ya-afya-kuimarisha-huduma-za.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/10/wizara-ya-afya-kuimarisha-huduma-za.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy